JUZ.1
Julai, 2014.
VYAKULA
NA VINYWAJI KATIKA UIMBAJI
Mhuville
Humphrey
1.0
Utangulizi
Uimbaji ni taaluma kama
zilivyo taaaluma zingine za sheria, elimu, uhandisi, usimamizi wa fedha,
biashara na kadhalika. Taaluma hizo na zingine zinautaratibu uliowekwa ili kumfanya
mtu asiyejua kujua na hatimaye kuitwa mwanasheria, mwalimu/mwezeshaji,
muhandisi au msimamizi wa fedha. Hivyo basi, uimbaji nao una taratibu zake hata
mtu akafikia kiwango cha kuthibitika kuwa ni muimbaji ama kwa kupewa cheti au
kuonesha uwezo wake mbele ya wengine; kanisani, kwenye majukwaa ya matamasha ya
uimbaji na kadhalika.
Kwahiyo, makala hii
imelenga kumsaidia muimbaji kumpa sheria na taratibu za uimbaji hususani katika
suala zima la chakula gani muimbaji ale au asile na vinywaji gani muimbaji
anywe au asinywe ili awe na uwezo wa kuimba vizuri mahali popote.
2.0
Nafasi ya Vyakula na Vinywaji katika uimbaji.
Katika suala la kula na
kunywa muimbaji yeyote anaweza kufananishwa na mkimbiaji. Mkimbiaji hawezi
kujishindilia chakula kingi au kunywa maji mengi wakati akijua anakwenda kwenye
mazoezi au mashindano ya kukimbia umbali wa maili fulani. Hii ni kwa sababu, atashindwa
kukimbia vizuri. Hata muimbaji; hawezi kula au kunywa kwa kupitiliza halafu asipate
shida wakati wa zoezi la kuimba. Hii ni kwa sababu, kushiba sana kunazuia zoezi
la upumuaji wakati wa uimbaji na kusababisha muimbaji kushindwa kutengeneza
sauti nzuri za uimbaji.
Pia, mkimbiaji hatokuwa
na nguvu za kukimbia kama hatokula chakula cha kutosha au kunywa maji ya
kutosha. Muimbaji halikadhalika, anahitaji kula chakula na kunywa maji kwa kuwa
uimbaji ni kazi ngumu ambayo inahitaji virutubisho vya kutia nguvu mwili ambavyo
vinapatikana katika vyakula na vinywaji tunavyotumia katika maisha yetu ya kila
siku. Hivyo, kula na kunywa ni jambo la muhimu sana kwa muimbaji katika zoezi
la uimbaji lakini kwa tahadhali.
2.1
Tahadhali ya vyakula na vinywaji katika uimbaji (nini muimbaji hapaswi kula au
kunywa katika siku ya uimbaji na wakati wa uimbaji)
Muimbaji asishinde na
njaa au kutokunywa maji kabisa siku ya uimbaji. Hii ni kwa sababu, kutokula
kutanyong’onyesha mwili wake hivyo atashindwa kuimba kwa ufanisi. Zingatia: kama muimbaji amefunga;
atumie maji (anywe kidogokidogo) ili kulainisha na kulifanya koo lake lisiwe
kavu. Pia, maji yatampa muimbaji nguvu
ya kusimama na kuwahudumia watu kwa muda uliopangwa.
Muimbaji asinywe
kinywaji chochote chenye kafeni. Hii hujumuisha vinywaji kama vile; kahawa,
cola (soda), chai ya rangi nyeusi (black tea) na vinywaji vyote ambavyo vina
cafeni ndani yake. Vinywaji hivi ni kichochezi cha mkojo na hufanya mwili wa
muimbaji kushindwa kufyonza maji kunakosababisha mwili kukauka au kuishiwa maji
ambayo ni muhimu sana katika kumpa muimbaji nguvu ya kuimba. Pia, vinywaji hivi
husababisha; kuzalishwa kwa kitu kama uteute (kamasi) kwenye kinywa na koo,
ukavu na maumivu kwenye koo, huleta kiungulia na kusababisha kucheua mara kwa
mara wakati wa uimbaji. Zingatia:
Kama muimbaji anashindwa kuacha vinywaji hivyo, inashauriwa kusukutua koo kwa
maji mara baada ya kunywa kinywaji cha namna hiyo kwa siku nzima ili kusafisha
koo na kuepuka athali zisababishwazo na vinywaji hivyo katika uimbaji. Pmoja na
hilo, muimbaji anywe maji mengi; zaidi ya glasi nane kwa siku. Au, Muimbaji
atumie chai nyeusi (black tea) ambayo inaelezwa kuwa na kiwango kidogo sana cha
kafeni. Ila matumizi ya chai ya kienyeji ni bora zaidi (mchaichai).
Muimbaji asile vyakula
au kunywa vinywaji vinavyoongeza au kuacha uteute kwenye kinywa na katika
koromeo kabla na wakati wa uimbaji. Mfano wa vyakula hivyo ni mayai, maziwa,
‘ice cream’ na bidhaa zingine za maziwa kama pipi, ‘chocolate’, biskuti, keki,
siagi, samri, koni na kadhalika. Uteute unaosababishwa na vyakula na vinywaji
hivyo huzuia utokaji mzuri wa sauti ya uimbaji wakati wa kuimba. Ndio maana
utakuta waimbaji wengine wanahama funguo za muziki au kushindwa kuimba sauti za
funguo za juu au kupata tatizo la kushindwa kupanda na kushuka vema kwa sauti
wakati wa uimbaji.
Muimbaji asitumie
vyakula au vinywaji vinavyokausha koo. Mfano wa vinywaji hivyo ni kama vile;
pombe, matunda jamii ya ndimu kama chungwa, limao, chenza, daransi, embe
mbichi, na kadhalika. Kukauka kwa koo kutasababisha sauti ya muimbaji kutotoka
vema kwasababu koo lake ni kavu.
Muimbaji asitumie soda
na vinywaji vyovyote vinavyotoa povu wakati vinapofunguliwa. Vinywaji hivi
huweka gesi/hewa tumboni na kumfanya muimbaji kubeu na/au kucheua hovyo na kusababisha
muimbaji kupata shida wakati wa kuimba na kutoa sauti mbaya.
Muimbaji asile vyakula
ambavyo vitaacha vitu kama makapi kwenye koo lake. Vyakula hivyo ni kama vile;
bisi, mahindi, karanga, tambi kavu, chama, na kadhalika. Ulaji wa vyakula hivi
kabla na wakati wa kuimba husababisha ugumu wa utoaji wa sauti za kuimbwa. Pia,
makapi hayo wakati mwingine hurukia katika koo la chakula na kusababisha
muimbaji kupaliwa na hatimae muimbaji kushindwa kupumua vema, kukohoa na kuimba
vibaya.
Muimbaji
asile vyakula vya mafuta sana kama vile nyama zilizonona na kadhalika. Pia,
sukari nyingi haifai kwa muimbaji.
Muimbaji
asile vyakula au vinywaji vinavyoleta mwasho au kukera koo (throat irritants),
vinavyochangamsha, kusisimua au kulewesha (Overly spicy foods) kama vile;
kahawa na pilipili, vinywaji baridi sana, sukari iliyosafishwa, chocolate na
kadhalika.
Muimbaji asitumie Jamii ya vitu vyenye
alkoholi, Sigara, tumbako, bangi, ugoro na aina yoyote ya madawa ya kulevya
kwakuwa vinaathali kubwa kwenye koo na mapafu ambavyo ni viungo muhimu sana katika
utengenezaji wa sauti bora za uimbaji.
Muimbaji asitumie
vyakula vyenye madhara kwa mwili wake (mzio; allege). Kwa mfano, baadhi ya
waimbaji hupata shida baada ya kula matunda jamii ya machungwa, ngano, karanga,
samakigamba, soya na kadhalika.
Muimbaji asitumie vyakula
vyenye mafuta mengi, na nyama nyekundu kama ya ng’ombe, mbuzi na kadhalika.
2.2
Vyakula na vinywaji vitakavyofanya muimbaji aimbe vizuri (vyakula na vinywaji
ambavyo muimbaji anashauriwa kuvitumia kabla na /au wakati wa uimbaji)
Muimbaji ale chakula
cha wastani (kiwango cha kutosheka) masaa mawili kabla ya uimbaji. Hii
itasaidia chakula kumengenywa vema na kumpatia muimbaji nguvu wakati wa kuimba.
Kushiba sana (kuvimbiwa) husababisha tumbo kushindwa kumeng’enya chakula kwa
haraka na hivyo kutamfanya muimbaji ashindwe kutoa sauti vema. Hii ni kwa
sababu, tumbo litashindwa kusukuma hewa kutoka nje ili kutengeneza sauti nzuri
za uimbaji. Pia, muimbaji atakuwa anabeua na kucheua hovyo wakati wa kuimba
hali ambayo humfanya kutoa sauti mbaya au kushindwa kuimba kabisa.
Muimbaji anywe maji ya
kawaida (room temperature water) yaani yasiwe ya moto wala ya baridi au barafu.
Maji hayo yanywewe masaa mawili kabla ya uimbaji. Maji haya yatampa nguvu
muimbaji, yatafanya koo la muimbaji kuwa bichi (sio kavu) na mwili kutokuwa
mkavu. Muimbaji hanabudi kutambua kuwa matumizi ya maji ya moto hutanua na maji
ya baridi (au barafu) husinyaza/hubana koromeo hivyo kusababisha kiboksi cha
sauti kushindwa kutengeneza sauti za kuimba vizuri na muimbaji ataimba vibaya. Zingatia: Unaweza kunywa maji ya moto
au ya baridi baada ya uimbaji na sio kabla au wakati wa uimbaji.
Muimbaji ale matunda
yenye maji mengi kwa ajiri ya kuufanya mwili wake kufyonza maji na kupata
nguvu. Mfano wa matunda hayo ni pamoja na tikiti maji, tango na kadhalika.
Muimbaji ale mboga za
majani zenye maji mengi kwa ajiri ya kuufanya mwili kupata maji, chumvichumvi
na madini ambavyo vyote ni virutubisho vitakavyompa muimbaji nguvu ya kuimba na
kutoa sauti yake vizuri wakati wa kuimba. Mfano wa mboga hizo ni pamoja na
mchicha, tembele, ‘spinach’, ‘chinise’, na kadhalika.
Muimbaji anaweza kutumia asali, na
chumvi kidogo ni nzuri kwa koo la lake katika siku ya uimbaji.
Matumizi ya chai ya
mitishamba (mchaichai) ni bora zaidi kwa afya ya koo na tumbo lako ili kusaidia
utengenezaji wa sauti nzuri za uimbaji.
3.0
Hitimisho na mapendekezo.
Koo hupendezwa, hutulizwa, huburudishwa,
hutengenezwa na aina fulani ya pipi, asali, mvuke,
chai ya mitishamba (mchaichai), kusafisha koo kwa maji chumvi, baadhi ya dawa
kwa ushauri wa daktari, unywaji wa maji, na kadhalika. Pia, kinyume chake koo
laweza kuharibiwa na matumizi ya vyakula au vinywaji kama vile; pombe, kahawa,
soda, maziwa, chokoleti, pipi, ubuyu, matunda jamii ya ndimu, mayai, karanga,
mahindi, bisi na kadhalika. Hivyo, muimbaji awe na taadhali katika matumizi ya
vyakula na vinywaji ili kufanya sauti yake kuwa bora na kupendeza mbele za watu
na Mungu tunayemtukuza kupitia sauti zetu.
Mathalani, mwanafunzi
mzuri ni yule anayetafuta zaidi maarifa mara baada ya kujifunza jambo fulani.
Hivyo, ni matumaini yangu kuwa mafunzo haya yatakuwa msingi bora kwa muimbaji
kutafuta zaidi kwa habari ya vyakula na vinywaji katika uimbaji. Haya
yalioelezwa hapa ni machache sana.
Pamoja na hayo, mabadiliko
chanya ya uimbaji yatategemea uzingativu na utekelezaji kwa vitendo wa mambo
hayo na sio kusikiliza tu. Pia, mabadiliko hasi yatatokea kwa wasiozingatia na
kutekeleza kwa vitendo mambo hayo. Yuko mshairi anasema,
“Mshumaa
tuliwasha, ili nuru kumulika,
Giza
kulitokomesha, na nuru kuenezeka,
Mshumaa unawaka,
giza mbona linazidi?”
Pia, mshairi mwingine
anasema,
“Mnazi
walioukwea,
Shinani
wameanzia,
Si kama
mejirukia,
Kileleni taka
tua,
Jikazie yako kwego, mnazi upate
kwea.”
Hivyo, huu ni mwanzo wa
kujifunza uimbaji; huna budi kuifuata nuru (mafunzo) unayoangaziwa (kupewa) ili
ufanikiwe katika uimbaji. Hii ni kwa sababu, wote waliofanikiwa katika aina
yoyote ile ya huduma, walianzia chini na kwa kuwa walisikiliza na kutekeleza
waliyoelekezwa na viongozi wao wakaweza kupanda na leo hii ni watu wakuu katia
huduma.
Mithali 4:10, 13, 18,
19, 20, 21, na 22 inasema,
“10 Mwanangu,
sikiliza, na kuzipokea kauli zangu; Na miaka ya maisha yako itakuwa mingi…
13 Mkamate sana
elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako…
18 Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing'aayo,
Ikizidi kung'aa hata mchana mkamilifu.
19 Njia ya waovu ni kama giza; Hawajui ni kitu
gani kiwakwazacho.
20 Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio
lako, uzisikie kauli zangu.
21 Zisiondoke machoni pako; Uzihifadhi ndani
ya moyo wako.
22 Maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya
ya mwili wao wote.”
Hivyo, ni vema
kuyafuata, kuyazingatia na kuyatendea kazi maarifa yote uliyopewa ili ufanikiwe
kiuimbaji kwani asiyefuata hayo anafananishwa na kama vile inavyofafanuliwa na
mwandishi wa Mithali 1:7b; anasema,
“Kumcha Bwana ni
chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu
hudharau hekima na adabu.”
Mhuville Humphrey, Mwl. Kiongozi -
Kusifu na Kuabudu ECWC-Mji wa Bwana Mbezi
0652 516 581/0685736581
BAed-St. John’s University of Tanzania
2011/2014
As ante sana nimekuelewa je na Maji ya vuguvugu nayo yanafaaa?
JibuFutaMazoezi pia Ni ya muhimu ktk uimbaji kutegeneza pumuzi ya kutosha
FutaMaji yeyote tu kwasababu kinachohitajika ni unyevu kooni yani ya viguvugu au yasiyovuguvugu.
FutaMaji yeyote tu kwasababu kinachohitajika ni unyevu kooni yani ya viguvugu au yasiyovuguvugu.
FutaMaji yeyote tu kwasababu kinachohitajika ni unyevu kooni yani ya viguvugu au yasiyovuguvugu.
FutaNimepata fundisho mm Kama muimbaji katika swala la kunywa na kula vyakula ambavyo vitamfanya mtu aimbe vizuri
JibuFutaNa vipi kuhusu mayai mabichii hii miekaaje?
JibuFutaVp kuhusu mayai kama alivyo uliza ndg hapo juu
JibuFuta"je, yanatumiwaje ?"
Ahsante sana ila nimetiya swali hapo juu👆👆👆
JibuFutaAhsante sana ila nimetiya swali hapo juu👆👆👆
JibuFutaVp kuhusu mayai kama alivyo uliza ndg hapo juu
JibuFuta"je, yanatumiwaje ?"
Swali lingine ni : "Vp kuhusu maji ya moto na asali kwa pamoja ?"
JibuFutaAmen ubarikiwe
JibuFutaVp kuhusu kunywa vinywaj vya baridi kupi
JibuFutata kias je hilo haliwez kuwa tatizo kwa muimbaj
Naomba kuuliza nizoezi gani lakuifanya sauti yangu ijae au iwe nauzito
JibuFutaImekaa vizuri elimu iongezwe zaidi ili tutambue jinsi ya kuweza kupafom vizuri hilo la mayai tupeni mawlekezo mliotutangulia ktk huduma hii jamen
JibuFuta